MSHUKIWA WA MAUAJI YA FAITH MUSEMBI MWANAFUNZI WA MKU AKAMATWA THIKA

Polisi mjini Thika wamemkamata mwanafunzi wa umri wa miaka 25 kutoka Chuo Kikuu cha Tom Mboya kuhusiana na mauaji ya mpenzi wake, Faith Musembi mwenye umri wa miaka 19.
David Kioko alikamatwa baada ya uchunguzi wa awali kupendekeza kwamba alimuua Faith kwa madai ya kutokuwa mwaminifu.
Inaarifiwa kwamba Faith Musembi alikujwa na ujauzito wa miezi nane kabla ya kukumbana na mauti.
Mwili wake ulipatikana na babake marehemu katika chumba chake cha kukodi pilot Estate mjini Thika kaunti ya Kiambu.