#Local News

MPOX YARIPOTIWA TENA NCHINI

Kisa cha tatu cha virusi vya nyani yaani Mpox kimeripotiwa nchini, huku mkurugenzi mkuu wa afya Dakta Patrick Amoth akisema mwathiriwa ni wa kike mwenye umri wa miaka 30 aliyekuwa amerejea jijini Nairobi baada ya safari nchini Uganda.

Kulingana na Amoth, mwathiriwa alirejea nchini baada ya safari ya wiki jana, na anapokea matibabu akiwa katika hali dhabiti.

Aidha, amesema watu 17 waliotangamana na mgonjwa huyo wanaendelea kufanyiwa uangalizi wa hali ya juu, na kuweka wazi kwamba mgonjwa wa pili amepona n akuruhusiwa kuondoka hospitalini.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *