WAKILI OMARI AOMBA MUKHWANA AACHILIWE KWA DHAMANA
Mawakili wa mmoja wa washukiwa katika kifo tata cha Albert Ojwang wakiongozwa na Danstan Omari wameitaka mahakama kumwachilia mshukiwa huyo James Mukhwana kwa dhamana.
Omari ameiambia mahakama kuwa afisa huyo wa polisi alijiwasilishwa baada ya kuhitajika na mamlaka ya Ipoa na kuwa yuko tayari kushirikiana na wanaoendesha uchunguzi.
Maafisa wa mamlaka ya Ipoa walikuwa wameomba kuzuiliwa kwa Mukhwana kwa muda wa siku 21 uchunguzi ukiendelea.
Imetayrishwa na Maureen Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































