#International #Local News

MPANGO WA HAITI WASITISHWA KWA WIKI TATU

Mpango wa kuwatuma maafisa wa polisi elfu 1000 wa kenya kuhudumu nchini Hait umeahirishwa kwa takribani wiki 3 ili kutoa nafasi kwa maafisa hao kuwa tayari kikamilifu.

Kundi la kwanza la maafisa hao likuwa linatarajiwa kuondoka kufikia mwisho wa mwezi huu baada ya serikali ya kenya kusisitiza kwamba mpango huo utaendelea licha ya msuko suko wa uongozi uilioshuhudiwa nchini Haiti vile vile pingamizi nchini Kenya.

Hatua ya kuahirisha mpango huo kwa wiki tatu unafuatia ziara ya utangulizi uliofanywa na maafisa 100 ambao waliekekea nchini Hait wiki jana na ambao wanaweka mikakati kabla ya kikosi kizima kuelekea huko.

Kikosi hicho cha maafisa 100 tayari kimefanya mikutano na vikosi vya vitengo vya usalama nchini Haiti ili kubaini mapengo ya kiusalama yaliyopo kabla ya kurejea kusubiri matayarisho ambayo yanajumuisha kutayarishwa kwa kambi zao na vile vile gala ya silaha.

Wakati wa mahojiano katika ziara yake ya marekani rais Ruto ambaye tayari amerejea nchini alizungumzia mpango huo kwa kina na kuutetea vikali akisema ni njia mojawapo ya kenya kuonyesha ushirikiano na mataifa mengine duniani.

Imetayarishwa na Janice Marete.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *