MSHUKIWA ‘ALIYELIPWA’ KUZIMA CCTV AKAMATWA
Mshukiwa wa pili katika uchunguzi wa mauaji ya bloga Albert Ojwang amekamatwa, taarifa zikiarifu kuwa mshukiwa huyo ni fundi wa mitambo anayedaiwa kuvuruga kanda za video za kamera za CCTV kwenye kituo cha polisi cha Central wakati wa tukio hilo.
Imearifiwa kuwa mshukiwa amekiri kulipwa shilingi elfu 3, kuvuruga kamera hizo na hivyo kutatiza Ushahidi unaoeweza kusaidia katika kuwawajibisha wahusika kwenye kesi hiyo.
Haya yanajiri baada ya kukamatwa kwa afisa wa polisi wa cheo cha konstebo James Mukhwana, anayehudumu katika kituo cha Central.
Imetayrishwa na Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































