#Local News

WAHUDUMU WA AFYA KAUNTI YA MIGORI WAHIMIZA WAZAZI KUPELEKA WANAO KUPOKEA ECDE

Idara ya Afya Kaunti ya Migori imetoa wito kwa wazazi walio na watoto walio na umri wa kati ya miaka 2 na sita kuwapeleka watoto wao kupokea virutubisho vya vitamini A hospitalini.

Hii ni katika juhudi za kudhibiti ongezeko la visa vya upungufu wa vitamini A katika kaunti hiyo.

Mtaalamu wa lishe katika Hospitali ya Rufaa ya Migori Steve Oyugi amesema chini ya asilimia 50 ya watoto walio na umri wa chini ya miaka sita wamepata nyongeza ya vitamini A katika Kaunti ya Migori.

Oyugi ameongeza kuwa wamejaribu kuwasiliana na wazazi wenye watoto walio na umri wa chini ya miaka sita lakini baadhi yao hawajaweza kuwapeleka watoto wao katika vituo vya afya.

Imetayarishwa na Janice Marete

WAHUDUMU WA AFYA KAUNTI YA MIGORI WAHIMIZA WAZAZI KUPELEKA WANAO KUPOKEA ECDE

KIPYEGON ARUDISHIWA NYOTA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *