#Football #Sports

NANJALA AREJEA NYUMBANI

Mshambulizi wa Harambee Starlets Violet Nanjala Wanyonyi ameamua kurejea kwenye klabu yake ya awali ya Municipal de Laayouyne nchini Morocco baadaya mpango wake wakujiunga na ligi kuu nchini Israel kufeli kutokana na changamoto za kiusalama.

Nanjala aliyechipuka kwenye shule ya upili ya Archibishop Njenga mjini Kakamega alikuwa amekamilisha mkataba na klabu moja ya ligi kuu ya soka la wanawake nchini Israel ila vita vinavyoendeea dhidi ya ukanda wa Gaza vimemfanya kubadili mawazo na kuamua kurejea kaskazini mwa bara Afrika alikohudumu kwa kipindi cha miaka miwili na kuibuka mfungaji bora.

Wanyonyi alijiunga na De Laayoune mwaka wa 2022 kwa mkataba wa miaka miwili nakusaidia timu hiyo kumaliza ya tatu katika msimu wake wa kwanza huku akiibukamfungaji bora na mabao 23 kwa mechi 26.

Wanyonyi aliyewahi kuchezea klabu za Trans Nzoia Falcons na Vihiga Queens kwa mkopo, atajiunga na klabu hiyo ya Morocco Agosti tarehe 29.

Imetayarishwa na Nelson Andati

NANJALA AREJEA NYUMBANI

POLICE BULLETS KUMENYANA NA RAYON SPORTS

NANJALA AREJEA NYUMBANI

MODO ANA IMANI NA KIKOSI CHAKE

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *