YAMAL NA WILLIAM WANG’ARA

Wachezaji nyota wa Uhispania Lamine Yamal na Nico Williams waling’ara huku La Roja ikiilaza Ufaransa 5-4 katika mchezo wa kusisimua mjini Stuttgart siku ya Alhamisi, na kutinga fainali ya Ligi ya Mataifa dhidi ya Ureno.
Yamal alifunga mabao mawili huku Williams akifunga na kutoa asisti wakati mawinga hao wawili wakikata safu ya ulinzi ya Ufaransa hadi kuwa riboni.
Mikel Merino na Pedri pia walikuwa kwenye ukurasa wa mabao kwa mabingwa hao wa Euro 2024. Kylian Mbappe alifunga penalti kipindi cha pili, lakini Uhispania walikuwa mbele kwa mabao 5-1, kabla ya Les Bleus kuamka ghafula huku wapinzani wao wakiondoa mguu wao kwenye kanyagio.
Mabao matatu ya dakika za lala salama ya Ufaransa – mshambulizi wa Rayan Cherki, bao la kujifunga la Uhispania na mkwaju wa dakika za lala salama kutoka kwa Randal Kolo Muani – hayakutosha.
Yamal, ambaye bado ana umri wa miaka 17, alisema Uhispania “ilistahili kushinda.”
Imetayarishwa na Nelson Andati