KALULU AJIUNGA NA JUVENTUS
Beki wa Ufaransa Pierre Kalulu amejiunga na Juventus kwa mkopo wa msimu mzima kutoka AC Milan.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ameichezea Milan mara 112 tangu aliposajiliwa mwaka 2020 baada ya kuhitimu kupitia akademi Lyon nchini ufaransa.
Juventus wana chaguo la kumnunua Kalulu kabisa mwisho wa mkopo wake.
Juve walianza kwa ushindi azma yao ya kunyakua taji la kwanza la Serie A tangu 2020 wikendi kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Como.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































