#Local News

NCIC YAWAITA WANASIASA WA TANA RIVER KUHUSU MAPIGANO YA KIKABILA

Wanasiasa watatu kutoka kaunti ya Tana River wamefikishwa mbele ya Tume ya Uwiano na Utangamano wa Kitaifa (NCIC) kuhusiana na mapigano ya kikabila yanayoendelea katika kaunti hiyo.

Watatu hao ni pamoja na aliyekuwa Mwakilishi wa Wanawake Rehema Hassan, Mbunge wa Galole, Hiribe Said Buya na mwakilishi wadi wa Bangale Jibril Mahamud, ambao waliitikia wito wa NCIC kuhusu mapigano hayo na wanatarajiwa kutoa mwanga zaidi kuhusiana na mapigano makali yanayohusisha koo mbili za makabila katika maeneo 12.

Kamishna wa NCIC Danvas Makori amesema viongozi hao watasaidia tume hiyo kutegua msingi wa mzozo ambao hadi sasa umegharimu maisha ya takriban watu 14.

Imetayarishwa na Janice Marete

NCIC YAWAITA WANASIASA WA TANA RIVER KUHUSU MAPIGANO YA KIKABILA

MGONJWA MMOJA WA MPOX AFARIKI DUNIA

NCIC YAWAITA WANASIASA WA TANA RIVER KUHUSU MAPIGANO YA KIKABILA

MICHANGO KWA SHIF NI YA LAZIMA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *