MAGAVANA WALAUMU RAIS RUTO
Baraza la magavana limemkosoa Rais William Ruto kutokana na kile wametaja kama kuleta uhasama kati ya magavana na wabunge, wakisema serikali kuu inawatumia wabunge kupunguza mgao wa kaunti huku ufisadi ukiongezeka kwenye serikali hiyo.
Haya yanajiri kufuatia kukamatwa kwa magavana George Natembeya na Kimani Wamatangi kwa tuhuma za ufisadi.
Kulingana na naibu mwenyekiti wa baraza la magavana Mutahi kahiga, kuna dhana kwenye taasisi mbali mbali za serikali kwamba kaunti hazitekelezi wajibu wake.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































