#Local News

KESI YA GACHAGUA YAAHIRISHWA IKISUBIRI MWELEKEO WA KOOME

Mahakama Kuu imeahirisha kesi ya kikatiba dhidi ya Rigathi Gachagua baada ya Mahakama ya Rufaa kubatilisha uteuzi wa jopo la majaji waliopaswa kusikiliza kesi hiyo, likisema ni Jaji Mkuu pekee mwenye mamlaka ya kufanya uteuzi huo.

Hata hivyo, katika taarifa iliyotolewa na Naibu Msajili Msaidizi Mheshimiwa Beja Nduke, pande zote ziliarifiwa kuwa kesi hiyo imeahirishwa hadi pale Jaji Mkuu atakapotoa mwelekeo zaidi.

Maendeleo haya yanajiri baada ya Mahakama ya Rufaa wiki iliyopita kubatilisha uamuzi wa Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu wa Oktoba 18, 2024 wa kuteua jopo la majaji watatu kusikiliza kesi hiyo.

Imetayarishwa na Janice Marete

KESI YA GACHAGUA YAAHIRISHWA IKISUBIRI MWELEKEO WA KOOME

HOJA YA KUTOKUA NA IMANI NA SASHA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *