#Basketball #Sports

EQUITY HAWKS WANUSI UBINGWA WA KITAIFA

Equity Hawks wamesalia hatua moja kutwaa taji la Ligi Kuu ya Kikapu ya Kitaifa ya Wanawake ya Kenya baada ya kuwalaza mabingwa watetezi wa Mamlaka ya Bandari ya Kenya (KPA) Jumapili kwenye Ukumbi wa Nyayo Gymnasium.

Wanabenki hao walilaza Dockers 66-64 katika Mchezo wa Pili kati ya msururu wa michezo mitano huku michezo mitatu iliyosalia ikipangwa kufanyika Mombasa wikendi ijayo.

Equity itatarajia kushinda mechi moja kati ya tatu zilizosalia ili kutawazwa mabingwa huku KPA ikilazimika kushinda michezo yote mitatu iliyosalia ili kutetea taji hilo kwa mara ya tatu mfululizo.

Wanabenki walishinda Mchezo wa Kwanza Jumamosi 67-62 kabla, kabla ya ushindi wa Jumapili.

Kocha mkuu wa KPA Anthony Ojukwu alikiri kuwa ilikuwa mechi ngumu lakini akaahidi fataki Mombasa watakapoikaribisha Equity.

Kwingineko katika fainali ya Ligi Kuu ya wanaume, timu ambayo haijashindwa Nairobi City Thunder pia inakaribia kushinda taji baada ya kushinda Mchezo wa Pili wa fainali ugenini mjini Mombasa.

Thunder aliishinda KPA 59-50 siku moja baada ya kushinda Mchezo wa Kwanza 73-70 katika mechi iliyochezwa katika Ukumbi wa Makande, Mombasa siku ya Jumapili.

Michezo iliyosalia itafanyika wikendi ijayo jijini Nairobi katika ukumbi wa Nyayo Gymnasium.

Imetayarishwa na Nelson Andati

EQUITY HAWKS WANUSI UBINGWA WA KITAIFA

SOFAPAKA WAGWARA NAIVAS

EQUITY HAWKS WANUSI UBINGWA WA KITAIFA

SPAIN WANGUKA NA EURO 2024

2 Comments

  1. Hey there just wanted to give you a quick heads up.

    The words in your post seem to be running off the screen in Chrome.

    I’m not sure if this is a formatting issue or something to do with internet
    browser compatibility but I figured I’d post to let you know.
    The layout look great though! Hope you get the issue
    resolved soon. Cheers

  2. Good info. Lucky me I found your blog by accident (stumbleupon).
    I have bookmarked it for later!

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *