BANDARI YA KISUMU YAENDELEA KUNG’ARA
Bandari ya Kisumu inazidi kuimarika kama kitovu cha biashara, baada ya kushuhudia ongezeko kubwa la meli na mizigo mwaka huu. Kwa mujibu wa KPA, bandari hiyo imeshughulikia tani 280,381 za mizigo mwaka 2025, ikilinganishwa na tani 116,578 mwaka uliopita.
Zaidi ya meli 67 zimezuru bandari hiyo, ikiwa ni pamoja na MV Orion II ambayo hivi karibuni ilipakia tani 600 za vigae kwenda Uganda. Mizigo mingi inayosafirishwa ni mafuta ya dizeli, vigae, chuma, na mbolea.
Miji inayofaidika zaidi ni Port Bell na Jinja nchini Uganda, pamoja na Mwanza nchini Tanzania. Meli saba sasa zinahudumu mara kwa mara katika bandari hiyo.
KPA imesema kuwa miradi ya uboreshaji wa miundombinu kama maghala na vifaa vya kisasa itaongeza uwezo wa Bandari ya Kisumu kukua zaidi kiuchumi.
Imetayarishwa na Mercy Asami
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































