MKURUGENZI WA WHO AITISHA MKUTANO WA DHARURA
Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani WHO Dkt.Tedros Adhanom Ghebreyesus ataitisha kamati ya dharura kufuatia ongezeko la ugonjwa wa M-pox,
Mkutano huo unatarajiwa kutoa mwelekeo iwapo mkurupuko huo ni dharura ya afya ya umma ya kimataifa na ikiwa ni hivyo itatoa ushauri mapendekezo ya muda ya jinsi ya kuzuia na kupunguza kuenea kwa ugonjwa huo.
Mkutano huo unajiri baada ya AFRICA CDC kutangaza M-pox kuwa dharura ya afya ya umma katika bara hili.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































