TUTAIMARISHA KIKOSI KWA MSIMU UJAO
Kocha mkuu wa klabu shiriki kwenye ligi ya NSL Naivas FC, Collins Omondi anasema anatanguliza kuimarisha safu yake ya ushambuliaji kabla ya msimu wa mwaka wa 2024-25.
Haya yanajiri baada ya vijana wake kukosa fursa ya kukwea daraja hadi ligi kuu kwa kulazwa jumla ya mabao 2-0 na Sofapaka kwenye mechi ya mikondo miwili ya mchujo.
Omondi, amesikitishwa kwamba washambuliaji wake hawakupata bao kwenye mechi ya mchujo baada ya kutengeneza nafasi nyingi katika mechi zote mbili.
Kulingana na mkufunzi huyo wa zamani wa Nairobi Stima, hakuelewa ni kwa nini wachezaji wake wanaweza kukosa kufunga hata bao moja licha ya kuwa na matokeo mazuri katika msimu uliomalizika hivi punde.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 

























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































