KUSHUTUMU URUSI NI UNAFIKI, GAVANA NASSIR

Siku moja baada ya rais William Ruto kulishutumu taifa la Urusi kuvamia Ukraine, gavana wa Mombasa Abdulswammad Nassir ameshtumu hatua hiyo akiitaja kuwa unafiki.
Kulingana na gavana huyo, msimamo wa rais Ruto unaoegemea upande mmoja, akizingatiwa kwamba kuna mapigano yanayoendelea katika mataifa mengine.
Aidha, amewataka wabunge kutilia maanani maslahi ya wananchi wakati wa kupitisha mswada wa kifedha wa mwaka 2024-25
Imetayarishwa na Antony Nyongesa