BABU OWINO AWASUTA POLISI KWA ‘KUMHANGAISHA’ WANJIGI

Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino amewashutumu maafisa wa polisi kwa madai ya kumhangaisha mfanyabiashara Jimi Wanjigi na familia ya mfanyabiashara huyo.
Akiwahutubia wanahabari, Babu ameitaja hatua ya maafisa wa polisi kuvamia makazi ya Wanjigi bila idhini ya mahakama kuwa kinyume na sheria.
Aidha, Babu ameunga mkono pendekezo la vijana wa Gen Z kuwasilisha hoja ya kuvunja bunge la kitaifa, kauli yake ikisisitizwa na mbunge wa Githunguri Gathoni Wamuchomba anayelihusisha bunge kuwa chimbuko la masaibu yanayolikumba taifa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa