AK YAFUNGUA OFISI ELDORET
Shirikisho La Riadha Nchini AK Limefungua Rasmi Ofisi Zake Katika Mji Wa Eldoret Ili Kuhakikisha Kuwa Huduma Zinawafikia Wanariadha Wengi Ambao Huishi Na Kufanya Mazoezi Katika Kaunti Za Kaskazini Mwa Bonde La Ufa.
Wakiongozwa Na Rais Wa Shirikisho Hilo Jackson Tuwei Na Mwenyekiti Wa AK Tawi La Nairobi Barnabas Korir, Viongozi Hao Wameisifia Hatua Hiyo Wakisema Ni Muhimu Katika Juhudi Za Kukuza Talanta Za Wanariadha Chipukizi.
Aidha, Wanariadha Nao Wamepongeza Hatua Hiyo Wakisema Kuwa Itawapa Afueni Kwa Kupunguza Safari Za Mara Kwa Mara Kuelekea Jijini Nairobi Kupokea Huduma Kama Vile Usajili, Kupata Stakabadhi Za Usafiri Miongoni Mwa Huduma Nyingine.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































