#Sports

ODEMBA KUONGOZA POLICE FC

Kocha wa Harambee Starlets, Beldine Odemba ataiongoza timu ya Ligi Kuu ya soka la wanaume Kenya Police FC dhidi ya Kariobangi Sharks katika mechi yao ya Jumamosi, baada ya kutimuliwa kwa Salim Babu na benchi lake zima la ufundi hapo jana.

Odemba, ambaye pia ni kocha mkuu wa Police Bullets, atasimamia upande wa wanaume kwa mechi ya wikendi pekee.

Polisi wamecheza mechi tano msimu huu, wakishinda moja, sare tatu na kufungwa moja.

Atakuwa mwanamke wa pili kuwa mstari wa mbele kuongoza timu ya wanaume katika mechi ya Ligi Kuu ya Kenya, baada ya Jackline Juma ambaye amekuwa akiifundisha FC Talanta tangu kuanza kwa msimu huu.

Imetayarishwa na Nelson Andati

ODEMBA KUONGOZA POLICE FC

JUHUDI ZA MASKAUTI KUIMARISHA LISHE POKOT

ODEMBA KUONGOZA POLICE FC

HAKUNA MALIPO KWAKO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *