#Rugby #Sports

ASATI APONGEZA KIKOSI CHAKE

Mchezaji wa wa timu ya KCB mchezo wa raga Samuel Asati amesema amefurahishwa na mpito mzuri kutoka raga ya wachezaji 15 hadi ya wachezaji saba saba anapoekea kuwailisha Kenya kwenye Michezo ya Olimpiki huko Paris, Ufaransa.

Akizungumza wakati wakiendelea kujiandaa na michezo hiyo katika kambi ya makazi ya timu hiyo iliyoko Miramas – Ufaransa, Asati anasema anafurahia msaada anaoupata kutoka kwa benchi la ufundi la timu hiyo na wachezaji wenzake.

Kwa hivyo anatazamia matokeo mazuri huko Paris.

Asati atakuwa mchezaji mbunifu wa timu hiyo huko Paris, jukumu ambalo anafurahia kucheza.

Kenya imejumuishwa pamoja na Samoa, Argentina na Australia na wanaamini wana kila kinachohitajika kuwakomesha wababe hao wa kimataifa.

Imetayarishwa na Nelson Andati

ASATI APONGEZA KIKOSI CHAKE

TUTAIMARISHA KIKOSI KWA MSIMU UJAO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *