#Local News

MAAGIZO MAPYA KWA POLISI, LSK IKIVUNA

Maafisa wa polisi wanaotumwa kuwakabili waandamanaji humu nchini watalazimika kuvalia sare rasmi za polisi mbali na kuhakikisha kuwa wanatambuliwa kwa urahisi, ikimaanisha kuwa hawaruhusiwi kuficha nyuso zao kwenye barakoa.

Ni uamuzi wa mahakama kuu kufuatia kesi iliyowasilishwa na chama cha wanasheria LSK kutokana na mauaji ya kijana Rex Maasai ambapo LSK ilidai afisa wa polisi aliyehusika na mauaji hayo hakuwa kwenye sare za polisi.

Kwenye uamuzi wake, jaji Bahati Mwamuye amesisitiza haja ya uwazi, uwajibikaji na haki ya wakenya kuwatambua maafisa wa polisi walio kwenye majukumu rasmi.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MAAGIZO MAPYA KWA POLISI, LSK IKIVUNA

RUTO AZUNGUMZIA MADENI VYUONI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *