#Football #Sports

GATUSSO AREJEA KIZIMBANI

Mchezaji wa zamani wa Harambee Stars Collins Okoth Ougo almaarufu Gattuso leo alifikishwa mahakamani pamoja na mshtakiwa mwenzake Silvia Aoko kuhusu mauaji ya mtoto mdogo katika mtaa wa Lucky Summer Estate, Ruaraka, Nairobi.

Wawili hao walifikishwa mbele ya Hakimu Alexander Muteti katika Mahakama ya Milimani lakini hawakujibu mashtaka hayo.

Upande wa mashtaka ulithibitisha kuwa washukiwa hao walikuwa wamefanyiwa matibabu, na Hakimu Muteti akaagiza ripoti za uchunguzi wa kiakili ziwasilishwe mahakamani kabla ya kujibu mashtaka mnamo Septemba 11, 2024.

Afisa wa Upelelezi, ambaye alifika mahakamani kufuatia wito wa mahakama, alikanusha madai kwamba alikataa kuachilia simu ya rununu na pesa za Bw. Okoth, ambaye alishiriki katika vilabu kadhaa vya Ligi Kuu ya Kenya kama mwanasoka.

Afisa huyo alifahamisha mahakama kuwa wakati wa kukamatwa, alipata simu ya mkononi aina ya Samsung na pochi iliyokuwa na vitambulisho viwili na kadi ya NHIF, na vyote vilirekodiwa katika orodha iliyotiwa saini na mshukiwa.

Okoth, kiungo mashuhuri wa zamani wa Gor Mahia na Harambee Stars, na mshtakiwa mwenzake Sylvia Aoko Odhiambo wanadaiwa kumuua msichana wa miaka mitatu, Pamela Atieno almaarufu Scovian Maya, Aprili 2024.

Imetayarishwa na Nelson Andati

GATUSSO AREJEA KIZIMBANI

USHINDI UMEIMARISHA KIKOSI

GATUSSO AREJEA KIZIMBANI

GAVANA LENOLKULAL APINGA HUKUMU

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *