KNUT, KUPPET WAONYA MGOMO UNGALIPO

Miungano ya kutetea maslahi ya walimu KNUT na KUPPET kutoka kaunti za Kericho, Kirinyaga na Kimabu imeapa kwamba walimu hawatarejea shuleni kwa muhula wa tatu unaoanza wiki ijayo iwapo serikali haitatekeleza mkataba wa maelewano.
Wakiongozwa na katibu mkuu wa KUPPET tawi la Kericho Mary Rotich, walimu wameilamu serikali kwa kukosa kutenga kima cha shilingi bilioni 13.3 za kufanikisha utekelezaji wa mkataba wa kati yam waka 2021- 2025.
Aidha, walimu hao wanashikikiza kuajiriwa kwa walimu zaidi ili kukabili uhaba wa walimu unaoshuhudiwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa