WATU 13 WAUAWA KATIKA MAANDAMANO
Watu 13 wamedhibitishwa kufariki dunia na wengine 150 kujeruhiwa katika maandamano huku mashirikia ya kutetea haki za binadamu yakiendeleza shutumu dhidi ya serikali kwa kutumia nguvu kupita kiasi.
Chama cha mawakili nchini LSK kikiongozwa na rais wao Faith Odhiambo kimeahidi kuwasaidia waadhiriwa wote kutafuta haki kwa wapendwa wao.
Hussein Khalidi mkurugenzi wa haki Afrika amesema kwamba kufikika jana watu kadhaa walikuwa wamethibitishwa kupigwa risasi na kuaga dunia.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































