TANGAKONA YA GIZA YAWATISHA WAKAZI

Wananchi katika kituo cha kibiashara cha Tangakona eneo bunge la Nambale Kaunti ya Busia wanahofia kwamba huenda hali ya usalama ikadorora nyakati za usiku baada ya taa za barabarani zilizowekzwa takriban miaka 10 iliyopita kutelekezwa.
Wakiongea katika soko hilo lililoko kwenye barabara kuu ya Busia kuelekea Mumias, wenyeji hao wakiwemo wahudumu wa boda boda wamesema kuwa hali hiyo inatishia kuangamiza biashara kutokana na ukosefu wa usalama.
Aidha, wametoa wito kwa mbunge wa eneo hilo Geoffrey Mulanya na Mwakilishi wa Wadi ya Nambale Mjini Ken Rubia kuingilia kati suala hilo.
Imetayrishwa na Antony Nyongesa