MWANAFUNZI AMCHOMA KISU MJOMBA WAKE NA KUTOROKA

Polisi wa Kadibo wanamsaka mwanafunzi wa miaka 19 anayedaiwa kumchoma kisu mjomba wake wa miaka 41 hadi kufa katika eneo la Ong’eche, Katho kaunti ya Kisumu
Inadaiwa mjomba huyo alisababisha mzozo baada ya kutaka kuchukua unga wa mahindi kwa nguvu, hali iliyomkasirisha msichanahuyo na kumchoma kisu kifuani.
Mshukiwa ametoroka baada ya tukio, na polisi wanaendelea na msako huku wakihimiza wananchi kutoa taarifa zitakazosaidia uchunguzi.
Imetayarishwa na Janice Marete