#Local News

315 WAMEANGAMIA KWENYE MAFURIKO, SERIKALI YASEMA

Watu 315 wameaga dunia kutokana na mafuriko hapa nchini, 38 hawajulikani waliko huku 293,205 wakiachwa bila makao baada ya makazi yao kusombwa na maji ya mafuriko.

Akiwahutubia waandishi wa habari katika jumba la Nyayo jijini Naiorbi, msemaji wa seriklai Isaac Mwaura, amesema wakenya takribani 306,522 wameathirika na mafuriko hayo, akitangaza kwamba kuna uwezekano mvua hiyo ikapungua katika maeneo mengi nchini.

Aidha, Mwaura amesisitiza msimamo wa serikali kwamba ziara ya rais kuelekea nchini Marekani kwa ndege ya kifahari ilifadhiliwa na serikali ya Uarabuni.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

315 WAMEANGAMIA KWENYE MAFURIKO, SERIKALI YASEMA

RUTO AZINDUA BWAWA LA KABKARA BUNGOMA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *