#Football #Sports

ADAM AANDIKA HISTORIA

Mwanalima Adam ameandikisha historia kwa kuwa Mkenya wa kwanza kucheza Ligi ya Taifa ya Wanawake (NWSL) nchini Marekani, akiwakilisha timu yake mpya, Kansas City Current.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 aliingia uwanjani katika dakika ya 65 akichukua nafasi ya Claire Hutton wakati tayari walikuwa chini kwa mabao 3-1.

Ingawa hajafurahishwa na matokeo hayo, anasema kuwa kucheza katika mojawapo ya ligi za soka za wanawake zenye ushindani mkubwa duniani ni ndoto kwake kutimia, na anafuraha kuitangaza Kenya kwenye jukwaa hilo la kifahari.

Uhamisho wake wa kihistoria kwa NWSL sio tu mafanikio ya kibinafsi lakini pia msukumo kwa wasichana wengi wachanga nchini Kenya na kote Afrika, ambao wanatamani kucheza kandanda katika kiwango cha juu zaidi.

Imetayarishwa na Nelson Andati

ADAM AANDIKA HISTORIA

WANJALA AJIUNGA NA ATHLETIC CLUB

ADAM AANDIKA HISTORIA

MWANIKI ATOLEWA NJE

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *