MWANAHARAKATI FREDRICK BIKERI AELEKEA MAHAKAMANI KUPINGA SHIF

Mwanaharakati Fredrick Bikeri, ameelekea kortini akitaka kuizuia serikali kuzindua mpango mpya wa Bima ya Afya ya Jamii utakaokuchukua nafasi ya NHIF.
Bikeri, anahoji kuwa kuna ukosefu wa uwajibikaji na mpito wa kiutaratibu kati ya NHIF na mpango mpya wa huduma ya afya wa serikali, Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii (SHIF).
Kupitia kwa Wakili Danstan Omari, mwanaharakati huyo anaeleza kuwa kukosekana kwa mabadiliko ya kiutaratibu kutumia SHIF kunaleta pengo kubwa na la janga katika sekta ya afya ambalo litasababisha kukatika kwa huduma za afya.
Imetayarishwa na Janice Marete