KIAMBU YAWATIMUA MADAKTARI
Mgomo wa madaktari katika kaunti ya Kiambu umechukua mkondo tofauti, baada ya serikali ya kaunti hiyo kuwafuta idadi ya madaktari isiyojulikana kwa madai ya kuhatarisha Maisha ya wagonjwa.
Tangazo la kuwafuta madaktari hao walioanza mgomo hapo jana limewekwa wazi na waziri wa afya kwenye serikali ya kaunti hiyo Elias Maina, zoezi la kuwahesabu madaktari ili kubaini ambao hawajaripoti kazini likiendelea.
Ameongeza kuwa serikali haitakubali sekta ya afya anayosema hupokea shilingi bilioni 8 kila mwaka kulemazwa
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































