MWENDESHA BODABODA AKAMATWA AKIWA NA SILAHA ZA KUTENGENEZA NYUMBANI
Mwendesha bodaboda na abiria wake wanaohusishwa na umiliki silaha ghafi wamekamatwa eneo la Dagoretti Corner jijini Nairobi.
Kulingana na ripoti ya polisi timu ya polisi ikiongozwa na kamanda wa polisi wa Riruta imeshika doria eneo la Dagoretti na kumwona mwendesha bodaboda huyo akielekea eneo la Fish Bay.
Kwa tuhuma, maafisa wamemsimamisha mwendesha bodaboda huyo ili kuwahoji zaidi, kabla ya kupata bastola kutoka kwa abiria huyo.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































