VYUO VIKUU KUANDAMANA KUPINGA MFUMO WA UFADHILI WA ELIMU YA JUU
Viongozi wa wanafunzi kutoka vyuo mbali mbali humu nchini wameendelea kuishinikiza serikali kubadilisha au kufutilia mbali kabisa mfumo wa ufathili wa elimu ya juu la sivyo watalemaza shughuli za masomo katika vyuo vikuu.
Wanafunzi hao wanapendekeza kupunguzwa kwa riba inayotozwa kwenye mikopo ya elimu ya juu kutoka asilim ia 4 hadi asilimia 2.
Iwapo matakwa hayo hayatatekelezwa wanafunzi hao wanasema kuwa watashiriki maandamano septemba tisa mwaka huu.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































