WIZARA YA MAZINGIRA IMETOA RATIBA YA KUENDESHA SHUGHULI YA UPANZI WA MICHE

Wizara ya mazingira imetoa ratiba kuhusu jinsi mawaziri watakavyoongoza shughuli ya upanzi wa miche kuanzia leo jumatatu.
Kwa mujimu wa wizara hiyo mwanasheria mkuu wa serikali Justin Muturi ataongoza shughuli ya upanzi wa miche katika msitu wa ngong kaunti ya Kajiado , naye waziri wa elimu Ezekieli Machogu ataongoza shughuli hiyo kesho jumanne katika kaunti ya Transnzoia.
Siku ya jumatano itakuwa zamu ya Waziri wa madini Salimu Mvuria katika kaunti ya tanariver kisha Waziri wa utalii Alfred Mutua ataongoza shughuli hiyo katika kaunti ya Kitui siku ya alhamisi kisha na hatimaye siku ya ijumaa wiki hii Waziri wa Kawi David Chirchir atakuwa kaunti ya Kericho na Baringo kwa shughuli ya upanzi wa miche kama walivyoagizwa na rais William Ruto ijumaa wiki iliyopita.