WATATU WALIOTOWEKA WAKATI WA MAANDAMANO WAPATIKANA KAJIADO

Watu watatu waliotoweka wakati wa maandamano ya Kitengela kaunti ya Kajiado ambao ni ndugu wawili na mwanaharakati mmoja, wamepatikana wakiwa hai
Watatu hao walitoweka tarehe kumi na tisa mwezi wa Agosti mwaka huu, wakati wa maandamano ya Gen Z ya kuishinikiza serikali iliyoko mamlakani kufanya mageuzi na kupunguza gharama ya Maisha. Gen Z walijitokeza pia kupinga sera za utawala wa Kenya Kwanza
Rais wa chama cha mawakili nchini, LSK, Faith Odhiambo amedhibitisha ndugu hao Jamil and Aslam Longton, wamepatikana katika eneo la Gachie kaunti ya Kiambu, naye Bob Njagi akipatikana pia akiwa hai eneo la Tigoni pia huko Kiambuu. Baba yake Longman Njagi amesema alipigiwa simu usiku na polisi wa Tigoni, wakimfahamisha kwamba Bob yuko hai.
Imetayarishwa na Kennedy Osoro