KIBERA SOCCER WOMEN, VIHIGA QUEENS FAINALI ZA FKF CUP
Warembo wa Kibera Soccer Women watamenyana na Vihiga Queens kwenye fainali za makala ya 4 ya kombe la FKF CUP mwaka huu kufuatia ushindi wao hapo jana.
Kibera Soccer Women wametinga fainali hizo baada ya kuwatandika mabingwa wa ligi kuu ya Kenya Police Bullets mabao 2:0 hapo jana, mabao hayo yakifungwa na Maximilla Munika na Faith Mboya, na kuzima ndoto ya Polisi Bullets kutwaa mataji mawili ya nyumbani.
Mkufunzi David Vijago, ameelezea furaha ya kuingia kwenye fainali hizo, akisema watajiliwaza na hatua hiyo licha ya kuangazia ubingwa wa ligi kuu.
Kwa upande wao, Vihiga Queens walicharaza malkia wenzao wa Bungoma Queens mabao 2:1, mabao ya Vihiga yakifungwa na Diana Cherono na Noel Amutata.
Hii itakuwa fainali ya pili kwa Vihiga Queens tangu mwaka wa 2023 walipopigwa mabao 2: 0 na Ulinzi Starlets.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































