SALASYA HURU TENA

Mbunge wa Mumias East Peter Salasya ameachiwa huru kwa dhamana ya shilingi elfu 200 baada ya kukesha kwenye seli za polisi wikendi nzima.
Salasya amefikishwa katika mahakama ya Milimani ambako amefunguliwa mashtaka ya uchochozi, mawakili wake wakidai kuwa haki zake zilikandamizwa wakati wa kukamatwa kwake.
Akizungumza na wanahabari nje ya mahakama, Salasya ameitaka idara ya polisi kutotumiwa kisiasa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa