RUTO, WENZAKE WASHTAKIWA MAHAKAMANI TANZANIA

Wanaharakati mbali mbali wameishtaki serikali ya kenya katika mahakama ya Afrika Mashariki nchini Tanzania kwa tuhuma za kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji walioshiriki maandamano ya kupinga mzigo wa ushuru mwezi jana.
Miongoni mwa washtakiwa kwenye kesi hiyo ni Rais William Ruto na naibu wake Rigathi Gachagua wanaotuhumiwa na ukiukaji wa haki za kibinadamu wakati wa kuwakabili waandamanaji.
Mmoja wa wanaharakati hao ni George Bush ambaye ni kiongozi wa bunge la wananchi, anayetaka watano hao kuwajibikia mauaji ya waandamanaji kibinafsi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa