UHISPANIA NDANI YA FAINALI
Uhispania walifunga mabao mawili ndani ya dakika tano katika kipindi cha kwanza na kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Ufaransa kwa bao la kuvunja rekodi kutoka kwa kijana Lamine Yamal na lengine la Dani Olmo na kuwafanya kutinga fainali ya Euro 2024.
Yamal mwenye umri wa miaka 16 alifuta bao la kwanza la Randal Kolo Muani kwa shuti zuri dakika ya 21 na kuwa mfungaji mwenye umri mdogo zaidi katika Euro au Kombe la Dunia kabla ya Olmo kuongeza jingine dakika ya 25 kwa bao lake la tatu katika hatua ya mtoano.
Sasa watamenyana na washindi wa mechi ya leo kati ya Uingereza na Uholanzi katika fainali mjini Berlin siku ya Jumapili huku wakiwinda taji la nne la Ulaya lililovunja rekodi.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































