KAPKEA KUPOKEA IDHINI KUWA NAIBU GAVANA

Bunge la kaunti ya Uasin Gishu limeratibiwa kumpiga msasa hapo kesho Evans kapkea aliyeteuliwa kuwa naibu gavana wa kaunti hiyo kujaza pengo lililoachwa na John Barorot aliyejiuzulu.
Gavana wa kaunti hiyo Jonathan Bii alimteua Kapkea mwenye umri wa miaka 34 na ambaye pia ni mwakilishi wadi ya Tembelio, na iwapo ataidhinishwa atakuwa naibu gavana wa 3 wa kaunti hiyo.
Barorot aliyejiuzulu baada ya kupata kazi katika shirika moja la kimataifa, aliondoka rasmi tarehe 31 mwezi jana.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa