CHELSEA BINGWA WA ULIMWENGU
Klabu ya Chelsea ya Uingereza ndiyo klabu bingwa ulimwenguni baada ya kutawazwa mabingwa hapo jana katika fainali ya kipute cha klabu bingwa ulimwengu yaani FIFA Club World Cup iliyoshirikisha klabu 32 kutoka mashirikisho ya mabara yote.
Hii ni baada ya Chelsea kuwacharaza mabingwa wa bara Ulaya Paris St Germain kwa mabao 3-0 katika uwanja wa Metlife Stadium, Cole Palmer akifunga mabao 2 ya ufunguzi ndani ya dakika 30 za kipindi cha kwanza, kabla ya Joao Pedro kufunga bao la tatu katika dakika ya 43.
Mchezaji Joao Neves wa PSG alipata kadi nyekundu ndani ya dakika 4 za mwisho baada ya kumvuta nywele mchezaji Cucurella.
Chelsea ambao ni washindi wa Conference League na waliomaliza nambari 4 katika ligi kuu ya Uingereza, mbali na kubeba taji hilo la FIFA, wamejipatia takriban Dola milioni 125.
Vilevile PSG watatuzwa kiasi hicho hicho licha ya kuwashangaza wengi kwa kichapo katika mechi hiyo iliyohudhuriwa na Rais wa Marekani Donald Trump.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































