WANAFAMILIA WANNE WAUAWA KATIKA SHAMBULIO LINALOSHUKIWA LA UCHOMAJI

Watu wanne wa Familia moja wameangamia katika ajali ya moto baada ya nyumba yao kuteketea huko Entara, Kaunti ya Kajiado alfajiri ya leo, katika shambulio linaloshukiwa la uchomaji moto.
Taarifa zinasema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa tisa asubuhi ya leo.
Familia hiyo, iliyojumuisha wanandoa na watoto wawili, wameteketezwa kiasi cha kutotambulika kabla ya moto huo kuzimwa na wakaazi wa eneo hilo.
Imetayarishwa na Janice Marete