CHELSEA YATELEZA KWA KICHAPO CHA 1-0 DHIDI YA ARSENAL

Chelsea ilipoteza 1-0 kwa Arsenal, ikiyumba katika mbio za kufuzu Ligi ya Mabingwa. Mikel Merino alifunga bao pekee dakika ya 20, akiipa Arsenal nafasi ya pili.
Chelsea ilimkosa Cole Palmer na haikuweza kutengeneza nafasi nyingi. Licha ya kubaki nafasi ya nne, ina ushindani mkali kutoka kwa timu tano zilizo karibu.
Mchezo ulikuwa na mashambulizi machache, hali inayoongeza shinikizo kwa kocha Enzo Maresca.
Imetayarishwa na Janice Marete