MABINGWA WAREJEA

Mabingwa wapya wa taji la raga shule za upili Afrika Mashariki All Saints na Kithimu Girls walirejea nyumbani mjini Embu kwa makaribisho mazuri baada ya kufanya vyema huko Bukedea, Uganda.
Walilakiwa kwa msafara wa magari uliopita katika mitaa ya mji wa Embu ukiongozwa na pikipiki kubwa la polisi.
Nahodha wa All Saints Brian Oyugi alihusisha mafanikio yao Afrika Mashariki na bidii kubwa.
All Saints walinyakua taji lao la kwanza la raga ya wachezaji 15 kwa ushindi wa 9-3 dhidi ya mabingwa watetezi St Mary’s Kisubi ya Uganda.
Kithimu Girls, pia kutoka Embu, waliwakilisha Kenya katika raga ya wachezaji saba lakini wakaondolewa kwenye mechi za mchujo.
Shule hizo mbili sasa zinasubiri mawasiliano rasmi kutoka kwa Wizara ya Elimu kuhusu iwapo serikali itafadhili timu hiyo kwa ajili ya Mashindano ya Dunia yanayopangwa kufanyika Monaco, Ufaransa baadaye Desemba.
Imetayarishwa na Nelson Andati