AFUENI: MATABIBU WASITISHA MGOMO
Ni afueni kwa wanaosaka huduma za kimatibabu katika hospitali za umma baada ya maafisa wakliniki kusitisha mgomo wao kwa siku 21 ili kupisha mazungumzo kuhusu malalamishi yao.
Katika taarifa kwa wanahabari, katibu mkuu wa muungano wa maafisa hao George Gibore hata hivyo, amesema mgomo huo utaendelea katika kaunti za Kwale, Vihiga, Uasin Gishu na Lamu.
Aidha, wamesisitiza kwamba ni sharti mkataba wakurejea kazini wa mwaka jana utekelezwe kikamilifu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































