NYORO: LISHE SHULENI INGALIPO
Mwenyekiti wa kamati ya bajeti katika bunge la kitaifa Ndindi Nyoro, amewahakikishia Wakenya kwamba mpango wa lishe shuleni ungalipo na kwamba serikali imetenga shilingi bilioni 3 kuwezesha mpango huo katika awamu ya kwanza.
Kauli yake imejiri baada ya kubainika kwamba hazina ya kitaifa imeondoa mpango huo kwenye makadirio ya bajeti ya mwaka wa kifedha wa 2024-2025, na kuzua mjadala mkali huku wakenya wakiishutumu serikali kwa madai ya kutowajali watoto.
Aidha, Nyoyo amesema kamati yake imetoa fedha za kutosha kufanikisha zoezi la kuwaajiri walimu wa JSS.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































