#Football #Sports

KENYA U-20 KUKABILI KUNDI GUMU AFCON MISRI

Timu ya taifa ya vijana wa chini ya miaka 20 itakabiliana na Nigeria, Tunisia na Morocco kwenye kundi gumu katika michuano ya AFCON ya mwezi huu nchini Misri.

Kenya, chini ya kocha Salim Babu, itashiriki kwa mara ya kwanza huku wapinzani wao wakiwa na uzoefu mkubwa.

Nigeria ni mabingwa mara saba na wamewahi kushiriki Kombe la Dunia la U-20 mara 13.

Morocco walitwaa taji lao pekee mwaka 1997, huku Tunisia wakimaliza nafasi ya pili mwaka 1985 na ya nne mara mbili, ikiwemo kupigwa 4-0 na Nigeria mwaka jana.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *