#Football #Sports

GUARDIOLA AKEMEA UDHAIFU WA MAN CITY BAADA YA KIPIGO CHA 5-1

Pep Guardiola amekemea “udhaifu” wa Manchester City baada ya kushindwa kujizuia na kufungwa 5-1 na Arsenal jana Jumapili.

City walirejea mchezoni kupitia bao la Erling Haaland baada ya Martin Odegaard kufunga mapema, lakini Arsenal walitumia makosa ya Phil Foden na John Stones kuwazidi nguvu.

Myles Lewis-Skelly, Kai Havertz, na Ethan Nwaneri walizidi kuufichua udhaifu wa safu ya ulinzi ya City, huku Guardiola akikiri kuwa wachezaji wake walijisababishia kipigo hicho.

Ilikuwa siku mbaya kwa City, wakionyesha ushambuliaji hafifu, kiungo kisicho na nguvu, na ulinzi dhaifu.

Imetayarishwa na Janice Marete

GUARDIOLA AKEMEA UDHAIFU WA MAN CITY BAADA YA KIPIGO CHA 5-1

KENYA PRISONS YASHINDA KAPU KATIKA MTANANGE MKALI

GUARDIOLA AKEMEA UDHAIFU WA MAN CITY BAADA YA KIPIGO CHA 5-1

KATE OSAMOR ATEULIWA KUWA MJUMBE WA BIASHARA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *