UTEUZI WA MWAURA KRA WABATILISHWA
Mahakama kuu imefutilia mbali uteuzi wa Anthony Mwaura kuwa mwenyekiti wa mamlaka ya ukusanyaji ushuru KRA ikitaja uteuzi huo uliofanywa na Rais William Ruto kuwa kinyume na katiba.
Katika uamuzi huo, jaji Francis Gikonyo amesema uteuzi huo ni kinyume na sura ya 6 ya katiba kuhusu maadili kwani Mwaura anakabiliwa na kesi ya ufisadi inayohusu shilingi milioni 357.
Kesi ya ufisadi dhidi yake iko mahakamani.
Imetyarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































