#Local News

KINDIKI AENDELEA KUMWITA MUSYOKA SERIKALINI

Naibu Rais Kithure Kindiki ameendeleza juhudi zake za kuitafutia serikali uungwaji mkono wa kisiasa kutoka eneo la Ukambani, akimtaka kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka ajiunge na serikali ya Kenya Kwanza.

Akizungumza baada ya kufanya mkutano na zaidi ya wawakilishi wadi 100 kutoka kaunti za Makueni, Machakos na Kitui, Kindiki amemtaka Musyoka kujiepusha na mrengo ambao kulingana naye, unaendeleza siasa za migawanyiko na ukabila.

Amewataka viongozi wa eneo hilo kushirikiana katika utekelezaji wa miradi ya serikali.

Imetayrishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *